MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester United imeingia mazima katika mbio za kumsajili kiungo wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni.
Kwa taarifa zilizopo, Man United imeshatenga dau nono la Pauni milioni 78 (zaidi ya Sh bil. 270 za Tanzania) kwa ajili ya Mfaransa huyo.
Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa habari za michezo, Eduardo Inda, tayari Man United wameshapeleka ofa hiyo Santiago Bernabeu.
Hata hivyo, huenda isiwe rahisi kwa Madrid kumwacha Tchouameni majira haya ya kiangazi.
Ni kwa sababu nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ni sehemu muhimu ya mipango ya msimu ujao ya kocha mpya, Xabi Alonso.
Wakati huo huo, inaelezwa kuwa Man United wako mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Brentford, Bryan Mbeumo.
Published:


