17.4 C
New York

Modric, Milan dili limeiva

Published:

MILAN, Italia
KOCHA wa AC Milan, Massimiliano Allegri, amefichua kuwa kiungo aliyeaga Real Madrid, Luka Modric, atajiunga na klabu hiyo ya Italia.
Kwa mujibu wa Allegri, ‘mido’ huyo wa kimataifa wa Croatia atajiunga na Milan baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Miezi miwili iliyopita, ilifichuka kuwa Madrid hawana mpango wa kumpa mkataba mpya nyota huyo.
Modric, staa wa zamani wa Tottenham ya Ligi Kuu ya England, alijiunga na ‘Blancos’ mwaka 2012.

Related articles

Recent articles