13.9 C
New York

Durant aondoka Phoenix, atua Houston

Published:

LOS ANGELES, Marekani
STAA wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), Kevin Durant, amejiunga na Houston Rockets akitokea Phoenix Suns.
Durant ameiacha Phoenix baada ya kuipa taji moja la NBA katika misimu yake mitatu klabuni hapo.
“Muda wangu hapa Phoenix umefikia ukomo. Kila nilichopitia hapa kimekuwa na faida kubwa kwangu,” alisema Durant.
Akiwa na Phoenix, Durant ambaye huu ni msimu wake wa 17 akiwa NBA, aliwahi kufunga pointi 26.8 katika mchezo mmoja.
Kwa kufanya hivyo, alivunja rekodi iliyokuwa imedumu kwa miaka zaidi ya 50.
Houston inakuwa klabu yake ya sita. Zingine ni Seattle, Oklahoma City, Golden State na Brooklyn.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img