Na Mwandishi Wetu
Kuelekea pambano la Dar Boxing Derby, bondia Iddi Pazi wa Chanika , ametamba kumchapa mpinzani wake Viguro Shafii wa Mabibo watakapopanda ulingoni Julai,2025 jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo, Pazi amesema moja ya sifa yake ni nguvu nyingi, hivyo atahakikisha anakua mshindi.
“Shafii ajiandae kwa kipigo kikubwa sana maana hajawahi kukutana na mabondia wagumu, sasa hapa anakutana na bondia na anaenda kupigwa vizuri tu. Mimi niko fiti na watu wangu wote,” amesema.
Kwa upande wa mashabiki na wa bondia huyo wamesema wanamuamini kutokana na rekodi zake mapambano yaliyopita.


