18.2 C
New York

Polisi Moshi wamsaka aliyejeruhi, kubaka

Published:

Na Yese Tunuka, Gazetini

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema msako wa kumtafuta mtuhumiwa aliyevamia na kujeruhi mabinti mawili, na kisha kumbaka mmoja.

Ni baada ya tukio la mabinti wawili, mmoja wa umri wa miaka 13 na mwingine miaka nane, kukatwa vidole baada ya kushambuliwa na mwanaume anayedaiwa kuvamia nyumba waliyokuwa wamelala katika Kitongoji cha Mtemboni, Himo, wilayani Moshi.

Katika tukio hilo la usiku wa kuamkia juzi Novemba 3, 2026, mwanaume huyo aliingia ndani ya nyumba hiyo kupitia dirishani baada ya kukata nondo, kisha kuwatishia watoto hao kwa kisu ili wasige kelele.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, mwanaume huyo aliwajeruhi watoto hao walipojaribu kujitetea, na ndipo alipofanikiwa kumchukua mkubwa na kwenda naye kwenye jengo ambalo ujenzi wake haujakamilika na kisha kumbaka.

Aidha, binti wa miaka nane anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Faraja, wilayani Moshi, huku anayedaiwa kubakwa akirejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

Related articles

Recent articles