RABAT, Morocco
FAINALI za Kombe la Dunia za soka la Wanawake wa U-17 zinaelekea ukingoni na zitahitimishwa kwa mchezo kati ya Nigeria na Japan.
Vijana wa Nigeria wamepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brazil na sasa wataivaa Japan katika mchezo wa fainali utakaochezwa Jumapili ya wiki hii mjini Rabat, Morocco.
Nigeria waliweza kuibana mbavu Brazil, kiasi cha kutokuipa hata shuti moja lililolenga lango katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
Bao lao la kwanza lilipatikana katika dakika ya 56 kupitia kwa Queen Joseph, kabla ya Awawu Bashiru kuongeza jingine dakika ya 71.
Bashiru alirudi kwenye nyavu za Brazil katika dakika ya 10, kisha Brazil kupata bao la kufutia machozi dakika ya 89.


