19.8 C
New York

Marekani yaipiga kufuli APR

Published:

KIGALI, Rwanda

TIMU ya mpira wa kikapu ya jeshi la Rwanda [APR] imezuiwa kushiriki Ligi ya Afrika ya mchezo huo [BAL], agizo hilo likitoka kwa waratibu ambao ni Marekani.

Chama cha Kikapu cha Marekani (NBA) ndicho kinachoandaa Ligi ya Kikapu ya Afrika na hatua ya kuizuia Rwanda kushiriki inatokana na uhusiano mbaya uliopo kati ya mataifa hayo.

Kwa mujibu wa NBA, APR iliyofanya vizuri mwaka jana na kushika nafasi ya tatu, haitotia mguu kwenye mashindano hayo kwa kuwa Taifa hilo liliwekewa vikwazo na Marekani.

Hatua ya NBA kuizuia APR imetokana na ombi la maseneta wawili wa Marekani waliotaka timu hiyo isipewe nafasi ya kushiriki BAL.

Marekani imekuwa ikilishutumu jeshi la Rwanda kwa kuchochea machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo [DRC].

Related articles

Recent articles