NEW YORK, Marekani
RAIA wa Haiti takribani 200,000 wameUmoja rejea nchini humo baada ya kukimbia mapigano ya magenge ya uhalifu yaliyotamalaki nchini humo.
Takwimu hizo ni za tangu kuanza kwa mwaka huu, zikiibuliwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) lililokutana jana Agosti 28, 2026.
Kikao hicho kimekuja zikiwa ni siku chache tu tangu mapigano ya magenge ya uhalifu yaliposababisha vifo vya wetu 47 mjini Port-au-Prince.
Kwa mujibu wa wanaharakati, Haiti iko kwenye hali mbaya ya usalama na mbaya zaidi haina rasilimali za kuzuia uhalifu unaoendelea.
“Kilichotokea hivi karibuni mjini Kenscoff ni mfano mdogo tu wa mateso wanayopitia raia wa Haiti kila siku,” amesema Naibu wa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, Indrika Ratwatte.


