LOS ANGELES, Marekani
UNAMFAFAMU Selena Gomez? Bibiye anayefanya vizuri kwenye soko la muziki nchini Marekani, pia akiwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa R&B, Justin Bieber.
Sasa, mrembo huyo anakabiliwa na skendo ya utapeli kupitia Kampuni ya Wondermind anayotajwa kuiasisi kwa lengo la kutoa sapoti kwa watu wenye changamoto ya afya ya akili.
Stori zinadai kuwa ni kampuni aliyoianzisha kwa kushirikiana na mama yake miaka mitano iliyopita, ingawa bibiye huyo amekana kuhusika nayo kwa namna yoyote ile.
Wawekezaji watano wamefungua kesi mahakamani wakidai kutapeliwa kiasi cha Dola milioni 1.2 walizoweka kwenye ‘projekti’ hiyo.
Selena kupitia kwa wanasheria wake, amekana kuhusika akisema madai hayo yamelenga kuichafua taswira yake.
Hata hivyo, wawekezaji wanadai kuwa waliweka fedha zao nyingi wakiamini Selena angeisimamia Kampuni hiyo akiwa mkuu wa Idara ya masoko.


