19.8 C
New York

Jesus sasa kutimkia Atletico

Published:

LONDON, Uingereza

MPACHIKAJI mabao wa Arsenal raia wa Brazil, Gabriel Jesus, yuko mbioni kujiunga na wakongwe wa La Liga, Atletico Madrid.

Mtaalamu wa habari za usajili nchini Hispania, Nicolo Schira, amedai kuwa Arsenal wako tayari kufanya biashara na Atletico.

Mkataba wa Jesus na Washika Bunduki hao wa London utafikia ukomo wake mwaka 2027 na hakuna mpango wa kupewa mwingine.

Nyota huyo ameshacheza mechi 123 tangu aliposajiliwa na Arsenal mwaka 2022 akitokea kwa wapinzani wao wakubwa, Manchester City.

Katika mechi hizo, Jesus ameweza kufunga mabao 32 na kutoa asisti 22 lakini kiwango chake kimekuwa kikipanda na kushuka kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Related articles

Recent articles