MONACO, Ufaransa
DROO ya ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2026-27 ilichezeshwa jana, Agosti 27, 2026 mjini Monaco, Ufaransa. Ligi hiyo kwa sasa inachezwa kwa mfumo wa Ligi, ikishirikisha timu 36.
Manchester United waliomaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England wakiwa nafasi ya tatu, wanashiriki kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa tangu michuano hiyo ilipoingia kwenye mfumo wa Ligi.
Mechi za kwanza zitaanza kuchezwa Septemba 8–10, 2026, kisha mwezi unaofuata, kwa maana ya Oktoba 13–14. Kwamba msimu utafikia ukomo wake Januari 27, 2027.
PSG
Katika mechi za nyumbani, itamenyana na Barcelona, Roma, Galatasaray na Slovan Bratislava, huku ikizifuata Manchester City, Aston Villa, Villarreal na Como ya Cesc Fabregas.
BAYERN MUNICH
Vigogo hao wa Bundesliga watakuwa na mechi zao za nyumbani dhidi ya Arsenal, Real Betis, Bodø/Glimt na Slavia Praha, kisha za ugenini dhidi ya Atlético Madrid, Manchester United, Lille na Viking.
REAL MADRID
Kwa mechi za nyumbani, wakongwe hao wa La Liga watakwaana na Inter, PSV, RB Leipzig na LASK, kisha wana michezo ya ugenini dhidi ya Arsenal, Roma, Shakhtar Donetsk na AEK Athens.
LIVERPOOL
Katika mechi zao watakazocheza Anfield, Liverpool watatoana jasho na Atlético Madrid, Porto, Villarreal na Lens, kisha za ugenini ni dhidi ya Inter, Club Brugge, Fenerbahçe na LASK.
INTER MILAN
Mechi zao za nyumbani ni dhidi ya Liverpool, Club Brugge, Shakhtar Donetsk na Stuttgart, halafu za ugenini ni dhidi ya Real Madrid, Borussia Dortmund, Feyenoord na Slovan Bratislava.
MANCHESTER CITY
Michezo yao ya nyumbani ni dhidi ya PSG, Sporting, Napoli, AEK Athens, kisha mechi za kwenda ugenini ni dhidi ya Barcelona, Porto, RB Leipzig na Lens.
ARSENAL
Walifika fainali msimu uliopita na safari hii mechi zao za ugenini ni dhidi ya Real Madrid, Borussia Dortmund, Lille na Sabah. Michezo ya ugenini ni dhidi ya Bayern Munich, Real Betis, Napoli na Slavia Praha.
BARCELONA
Mechi zao za nyumbani, Camp Nou, ni dhidi ya Manchester City, Aston Villa, Feyenoord na Como, kisha ugenini ni dhidi ya PSG, Sporting, Galatasaray na Sabah.
ATLETICO MADRID
Michezo watakayokuwa nyumbani ni dhidi ya Bayern Munich, Manchester United, Fenerbahce na Viking, na ile ya ugenini itawakutanisha na Liverpool, PSV, Bodø/Glimt na Stuttgart.
BORUSSIA DORTMUND
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Inter, Real Betis, Villarreal na AEK Athens, wakati zile za ugenini zitaikutanisha na Arsenal, Aston Villa, Bodø/Glimt na Sabah.
AS ROMA
Katika mechi zao nne za ugenini, Waitalia hao watakwaana na Real Madrid, Sporting, Lille na Slovan Bratislava, kisha ugenini watazifuata PSG, Manchester United, Fenerbahce na AEK Athens.
SPORTING LISBON
Watatumia uwanja wao wa nyumbani kumenyana na Barcelona, Manchester United, Galatasaray na LASK, halafu mechi za ugenini ni dhidi ya Manchester City, Roma, Shakhtar Donetsk na Lens.
ASTON VILLA
Mechi za nyumbani ni dhidi ya PSG, Borussia Dortmund, Fenerbahce na Viking, kisha za ugenini ni dhidi ya Barcelona, Club Brugge, Galatasaray na Slavia Praha.
PORTO
Katika uwanja wao wa nyumbani, Wareno hao watazikaribisha Manchester City, PSV, Napoli na Slavia Praha, kisha watazifuata Liverpool, Real Betis, Feyenoord na LASK.
MANCHESTER UNITED
Katika michezo minne ya nyumbani, ‘Mashetani Wekundu’ watazikabili Bayern Munich, Roma, RB Leipzig na Sabah, kisha mechi za ugenini ni dhidi ya Atlético Madrid, Sporting, Villarreal na Como.
CLUB BRUGGE
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Liverpool, Aston Villa, Bodø/Glimt na Lens, wakati zile za ugenini ni dhidi ya Inter, PSV, Napoli na Stuttgart.
REAL BETIS
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Arsenal, Porto, Feyenoord, Como, kisha zile za ugenini ni dhidi ya Bayern Munich, Borussia Dortmund, Lille na Slovan Bratislava.
PSV EINDHOVEN
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Atletico Madrid, Club Brugge, Shakhtar Donetsk na Stuttgart, na za ugenini ni dhidi ya Real Madrid, Porto, RB Leipzig na Viking.
FEYENOORD
Nyumbani wana mechi nne dhidi ya Inter, Porto, RB Leipzig, Como, kisha ugenini wanazo nne pia dhidi ya Barcelona, Real Betis, Galatasaray na Viking.
LILLE
Katika mechi za nyumbani ni dhidi ya Bayern Munich, Real Betis, Galatasaray na Slovan Bratislava, huku za ugenini zikiwa ni dhidi ya Arsenal, Roma, Bodø/Glimt na Stuttgart.
BODO/GLIMT
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Lille na LASK. Michezo yao ya ugenini ni dhidi ya Bayern Munich, Club Brugge, Napoli na Lens.
NAPOLI
Katika mechi za nyumbani, watazivaa Arsenal, Club Brugge, Bodø/Glimt na Viking. Michezo yao ya ugenini ni dhidi ya Manchester City, Porto, Villarreal na Sabah.
RB LEIPZIG
Michezo yao ya nyumbani msimu huu ni dhidi ya Manchester City, PSV, Shakhtar Donetsk na Lens. Katika mechi za ugenini, watazifuata Real Madrid, Manchester United, Feyenoord na Como.
VILLARREAL
Katika mechi za nyumbani, watakiwasha na PSG, Manchester United, Napoli na Sabah. Kwa upande wa ugenini, ni dhidi ya Liverpool, Borussia Dortmund, Fenerbahce na Slavia Praha.
FENERBAHCE
Mechi zao za nyumbani ni dhidi ya Liverpool, Roma, Villarreal na Slavia Praha. Michezo ya ugenini ni dhidi ya Atletico Madrid, Aston Villa, Shakhtar Donetsk na LASK.
SHAKHTAR DONETSK
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Real Madrid, Sporting, Fenerbahçe na AEK Athens, wakati za ugenini ni dhidi ya Inter, PSV, RB Leipzig na Slovan Bratislava.
GALATASARAY
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Barcelona, Aston Villa, Feyenoord na Stuttgart na za ugenini ni dhidi ya PSG, Sporting, Lille na AEK Athens.
SLAVIA PRAHA
Katika mechi za nyumbani, watacheza na Arsenal, Aston Villa, Villarreal na Lens na zile za ugenini ni dhidi ya Bayern Munich, Porto, Fenerbahçe na Sabah.
SLOVAN BRATISLAVA
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Inter, Real Betis, Shakhtar Donetsk na Stuttgart. Katika michezo ya ugenini watakiwasha na PSG, Roma, Lille na LASK.
STUTTGART
Katika mechi za nyumbani, watacheza dhidi ya Atlético Madrid, Club Brugge, Lille na Viking. Michezo ya ugenini ni dhidi ya Inter, PSV, Galatasaray na Slovan Bratislava.
AEK ATHENS
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Real Madrid, Roma, Galatasaray na LASK. Michezo yao ya ugenini ni dhidi ya Manchester City, Borussia Dortmund, Shakhtar Donetsk na Como.
LASK
Mechi zao za nyumbani ni dhidi ya Liverpool, Porto, Fenerbahçe na Slovan Bratislava. Michezo yao ya kwenda ugenini ni dhidi ya Real Madrid, Sporting, Bodø/Glimt na AEK Athens.
COMO
Katika mechi zao za nyumbani, watakwaana na PSG, Manchester United, RB Leipzig na AEK Athens. Michezo ya ugenini ni dhidi ya Barcelona, Real Betis, Feyenoord na Lens.
LENS
Katika michezo ya nyumbani, watacheza dhidi ya Manchester City, Sporting, Bodø/Glimt na Como. Mechi za ugenini ni dhidi ya Liverpool, Club Brugge, RB Leipzig na Slavia Praha.
VIKING
Katika mechi za nyumbani, watavaana na Bayern Munich, PSV, Feyenoord na Sabah. Mechi za ugenini ni dhidi ya Atlético Madrid, Aston Villa, Napoli na Stuttgart.
SABAH
Mechi zao za nyumbani ni dhidi ya Barcelona, Borussia Dortmund, Napoli na Slavia Praha. Kwa upande wa ugenini, watazifuata Arsenal, Manchester United, Villarreal na Viking.


