RIYADH, Saudi Arabia
NAHODHA wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo.
Ronaldo ameandika historia hiyo jana Agosti 28, 2026, baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Al-Taawoun.
Mreno huyo amefikisha mabao 104 ya Ligi Kuu akimzidi moja Mohammed Al-Sahlawi aliyekuwa kinara kwa mabao 103.
Ronaldo ameitumikia timu hiyo katika michezo 110 tangu alipojiunga nayo akiwa mchezaji huru aliyeondoka Manchester United.
“Nimefurahi sana. Ni mafanikio makubwa. Lakini, sio jitihada zangu pekee. Napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu, bila wao hakuna ambalo lingewezekana.


