22.2 C
New York

Chelsea na mkosi wa jezi namba 9

Published:

LONDON, Uingereza

ILIMCHUKUA sekunde 31 pekee straika wa Kibrazil, Joao Pedro, kuifungia bao Chelsea katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Fulham, mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) uliochezwa Jumatatu ya wiki hii, Agosti 24, 2026.

Hata hivyo, swali ni je; ataendeleza moto wake huo akiwa na jezi namba 9, ambayo imekuwa ikionekana kuwa na mkosi kwa mastraika wengi waliopita Stamford Bridge?

Tangu Jimmy Floyd Hasselbaink alipoondoka mwaka 2004, Blues haijapata mshambuliaji aliyeitendea haki jezi hiyo.

Didier Drogba alifanya makubwa klabuni hapo lakini alitumia jezi namba 11. Diego Costa naye alifanya vizuri akiwa na namba 19.

Kwa nyakati tofauti, washambuliaji wakubwa kama Romelu Lukaku, Alvaro Morata, Gonzalo Higuain, Radamel Falcao na Pierre-Emerick Aubameyang walifeli waikiwa na jezi namba 9.

Mshambuliaji wa mwisho kuvaa jezi hiyo kabla ya Pedro alikuwa Liam Delap na alimaliza msimu uliopita wa EPL akiwa amefunga bao moja pekee.

Kwa mashabiki wa Chelsea walio wengi, walau straika raia wa Uingereza, Tammy Abraham, alihitahidi akiwa na jezi hiyo, ingawa naye aliishia kutimkia AS Roma.

Pedro aazungumziaje nuksi inayohusishwa na jezi hiyo? “Siamini katika hilo. Sidhani kama namba zinaweza kuamua chochote,” alisema baada ya mchezo wao dhidi ya Fulham.

Msimu uliopita, Pedro alifanya vizuri akiwa na jezi namba 20. Alifunga mabao 20 pia katika mechi za michuano mbalimbali.

Tofauti na ilivyo kwa wengine, Pedro anatokea katika familia ya soka. Baba yake, Jose Joao de Jesus ‘Chicao’, alikuwa mchezaji wa Botafogo ya nchini kwao, Brazil.

Hata hivyo, Chicao aliwahi kuitumikia miaka nane gerezani kwa kesi ya mauaji, hivyo Pedro kubaki kwenye malezi ya mama na bibi yake.

Related articles

Recent articles