LOS ANGELES, Marekani
MAMILIONI ya wapenzi wa muziki wa Country kutoka pande zote za dunia wameguswa na kifo cha nguli Dolly Parton aliyefariki hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 80.
Mzaliwa huyo wa Milima ya Smoky Mountains, Tennessee, Marekani, atakumbukwa kwa ngoma zake zilizowahi kuitikisa dunia, zikiwamo ‘Coat of Many Colors’, ‘Jolene’ na ‘I Will Always Love You’.
Kwa miaka zaidi ya 70 ya maisha yake ya muziki, Dolly alishinda tuzo 10 za Grammy, akiuza nakala zaidi ya milioni 100 kupitia ngoma zake zaidi ya 3,000.
Katika mahojiano yake mengi, bi. Dolly alisisitiza mara kadhaa, kwamba muziki kwake si kazi, bali njia ya kuwasilisha hisia zake. “Ni njia yangu ya kujieleza. Ni tiba yangu,” alisema.
Nje ya muziki, Dolly pia alijipatia umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha televisheni alichofanya kwa miaka zaidi ya 60.
Jina lake halisi ni Dolly Rebecca Parton na alizaliwa mwaka 1946 akiwa wa nne katika familia ya watoto 12. Familia masikini iliyoishi kwenye nyumba ya chumba kimoja mjini Tennessee. Baba yake, Robert Lee Parton, alikuwa mkulima wa tumbaku.
Hata hivyo, familia ilikuwa na damu ya muziki kwani mama yake, Avie Lee, alikuwa mwimbaji na shangazi na mjomba walikuwa wapigaji wa gitaa.
Akiwa na umri wa miaka sita tu, Dolly alishaanza kuimba kwaya katika kanisa ambalo babu yake alikuwa mchungaji. Wakati huo pia, akawa anatumbuiza kwenye moja ya vipuindi vya televisheni.
Mwaka 1959, akiwa na umri wa miaka 13, Dolly alitumbuiza katika Ukumbi mkubwa wa Grand Ole Opry mjini Nashville, ambapo mjomba wake, Bill Owens, alimsindikiza kwa kupiga gitaa.
Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1964, alihamia Nashville na kuianza rasmi safari yake ya muziki. Huko ndiko alikokutana na Carl Dean, mwanaume ambaye walifunga naye ndoa miaka miwili baadaye. Hawakupata mtoto hadi Dean alipofariki mwaka 2025.
Kwa upande wa muziki, nyota ya Dolly ilianza kung’ara alipokutana na staa wa muziki wa Country, Porter Wagoner, ambaye alimuajiri kama mtumbuizaji katika shoo yake ya televisheni.
Miaka saba tu baadaye, Dolly na Wagoner wakawa na ‘pacha’ maarufu. Mbali na kuimba, Dolly akawa na uwezo mkubwa wa kutumia ala za muziki, zikiwamo ‘banjo’, ‘piano’ na ‘saxophone’.
Mwaka 1971, Dolly aliingia kwa mara ya kwanza kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya Grammy kupitia wimbo wake uliofanya vizuri wa ‘Joshua’. Miaka mitatu baadaye, akaachana na Wagoner na kuwa mwanamuziki wa kujitegemea.
Kupitia kitabu chake cha ‘Star of the Show: My Life on Stage’, Dolly anazungumzia kuachana na Wagoner akisema mwenzake huyo alianza kuyaona mafanikio yake kama tishio kwake.
Hata hivyo, Dolly aliachia wimbo maarufu wa ‘I Will Always Love You’ kama ujumbe wa kumwachia Wagoner. Inaelezwa kuwa Wagoner alilia baada ya kuusikia wimbo huo kwa mara ya kwanza. “Ni wimbo mzuri zaidi kuwahi kuusikia,” alisema Wagoner.
Akiwa peke yake, miongoni mwa ngoma zake kali ni ‘Jolene’ ulioingia sokoni mwaka 1974. Katika wimbo huo, anamzungumzia msichana wa benki anayetoka na mpenzi wake. Ikumbukwe, mume wake, Dean, naye alikuwa mfanyakazi wa benki wakati huo.
Hivyo, katika ngoma hiyo, Dolly anasikika akimbembeleza mwanamke (Jolene) anayefanya kazi benki kuachana na mpenzi wake (Dean). “Jolene, nakuomba, niachie mtu wangu,” anaimba Dolly katika wimbo huo.
Miaka ilivyozidi kusogea, ndivyo Dolly alivyozidi kuwa mkubwa kwenye kiwanda cha muziki ndani na nje ya Marekani na hatimaye akabeba tuzo yake ya kwanza ya Grammy mwaka 1978 kupitia wimbo ‘Here You Come Again’.
Kutokana na mapato ya muziki na biashara zingine, mwaka 2022, Jarida maarufu la Forbes lilimtaja Dolly kama mwanamke tajiri zaidi nchini Marekani. Utajiri usio wa kurithi. Mbali ya kuwa na lebo yake, Dolly Records, pia alimiki kampuni ya burudani ya Dollywood Company.
Dolly alisifika pia kwa jitihada zake za kuhakikisha jamii zinaondokana na tatizo la watu wake kutokujua kusoma na kuandika, kama ilivyokuwa kwa baba yake. Mwaka 1999, alifungua Maktaba kubwa mjini Tennessee.
Ni Maktaba ambayo imekuwa na matawi yake katika nchi zingine za Australia, Uingereza, Jamhuri ya Ireland na Canada, ikigawa mamilioni ya vitabu vya watoto kila mwaka.
Kupitia Taasisi yake ya Dollywood, aliweza kutoa ufadhili wa masomo, huduma za afya na kuchangia majanga ya mafuriko na moto kwa wenye uhitaji. Ni kama alivyochagia Dola milioni moja wakati wa Covid-19 mwaka 2020.
Katika miaka ya hivi karibuni, Dolly alihairisha shoo zake nyingi kutokana na changamoto za kiafya. Mei, 2026, alitangaza kusistisha shoo yake ya mjini Las Vegas kutokana na tatizo la mawe kwenye figo.
Tofauti na wanamuziki wengi, Dolly hakuwahi kujihusisha na siasa. Katika mahojiano yake, alizungumzia uamuzi wake huo akisema hataki kuwagawa mashabiki.


