19.6 C
New York

Ronaldinho arudi uwanjani, atua Italia

Published:

MILAN, Italia

MKONGWE wa soka la Brazil, Ronaldinho, amejiunga na klabu ya Ravenna inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Italia.

Ronaldinho (46), alistaafu mwaka 2015 lakini jana Agosti 20, 2026, alitangaza kurudi mzigoni baada ya miaka 11 ya kuwa nje ya soka la ushindani.

“Nimefurahi kuwa hapa na marafiki. Tuna timu yenye uwezo wa kupata mafanikio,” amesema wakati wa utambulisho wake klabuni hapo.

Ronaldinho alitwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 2002, tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2005, na alicheza mechi yake ya mwisho mwaka 2015 akiwa na Fluminense ya Brazil.

Nyota huyo amesema hajajua kama atacheza kikosi cha kwanza katika timu yake mpya kwani hiyo itategemea mipango ya benchi la ufundi.

Related articles

Recent articles