PARIS, Ufaransa
PSG imekamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Barcelona, Ferran Torres, na kumkabidhi jezi namba 9 klabuni hapo.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 26, amesaini mkataba wa miaka migano na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita (2025-26).
Ripoti zinaeleza kuwa PSG wamelipa Pauni milioni 43 kuinasa saini ya Torres aliyemaliza msimu huo akiwa amefunga mabao 21 na kutoa asisti tatu katika mechi 49.
Aidha, kusajiliwa kwa Torres kunafungua mlango kwa Bradley Barcola kuondoka PSG na kujiunga na vigogo wa England, Liverpool.
Barcelona imethibitisha kumuuza staa huyo kupitia taarifa yake, ikisema: “FC Barcelona na PSG zimefikia makubaliano ya uhamisho wa Ferran Torres kujiunga na klabu hiyo ya Ufaransa.”


