28.2 C
New York

Tetemeko la ardhi laua watu 47 Indonesia

Published:

JAKARTA, Indonesia

WATU takribani 47 wameripotiwa kupoteza maisha katika tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 lililotokea asubuhi ya leo Agosti 15, 2026, nchini Indonesia.

Kupitia taarifa yake rasmi, Shirika la Udhitibiti wa Majanga la Indonesia (BNPB) limethibitisha kutokea kwa tetemeko hilo katika Kisiwa cha Flores.

Katika taarifa yake, BNPB imeeleza kuwa mbali ya vifo hivyo, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kwa viwango tofauti, pamoja na mamia ya majengo kuharibiwa.

Video iliyosambaa mitandaoni na kuthibitishwa na mamlaka imeonesha jengo la kivuko likianguka kutokana na uzito wa tetemeko hilo.

Ifahamike kuwa Indonesia, moja ya nchi za barani Asia, imekuwa muhanga wa matukio ya matetemeko ya ardhi kwa miaka mingi.

Related articles

Recent articles