30 C
New York

Sekta za Mageuzi zinazoibeba Dira 2050: Utalii

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

Kama ilivyo kilimo, utalii ni sekta nyingine nyeti katika uchumi wa Tanzania. Kwa takwimu halisi, inachangia asilimia 25 ya mapato ya mauzo ya nje, hivyo ni moja ya sekta kuu za uchumi wa nchi.

Utalii unaendelea kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ukichochea sekta muhimu kama vile ukarimu, usafiri na biashara.

Kufikia waka 2050, utalii unatajiwa kuwa moja ya vyanzo vikuu vya ajira za moja kwa moja, huku fursa kubwa zikionekana katika sekta za ukarimu, kuongoza watalii, usafirishaji na biashara za ndani.

Sekta hii itapanuka zaidi na kuvutia wageni wa nje na ndani kupitia utalii unaohusisha utamaduni, urithi wa asili na malikale, utalii endelevu wa mazingira, utalii wa meli na fukwe, utalii wa uwindaji na mikutano na maonesho, na hivyo kuongeza mapato ya fedha za kigeni.

Hata hivyo, ukuaji huu utategemea uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu, utangazaji katika masoko lengwa, na ushirikishwaji wa jamii katika maeneo mbalimbali ya utalii.

Hivyo, ni muhimu kukuza utamaduni wa kutoa huduma bora ili kuimarisha utalii wa Tanzania. Kupitia hatua hizi, Tanzania inalenga kuwa kitovu cha utalii barani Afrika ifikapo mwaka 2050.

Related articles

Recent articles