23.1 C
New York

Gaza katikati ya matumani, giza la hofu

Published:

JERUSALEM, Palestina

KAULI ya Rais Donald Trump kwamba kundi la Hamas limekubali kuweka silaha chini limeibua matumaini kwa wananchi wa Palestina kuanza kuishi maisha ya amani katika Ukanda wa Gaza.

Kwa upande mwingine, bado wanatilia shaka uwezekano wa Israel na Hamas kumaliza vita, wakikumbuka kuwa ni mara kadhaa zimekuwa ahadi za aina hiyo lakini ziliota mbawa.

Oktoba, 2025, Israel na Hamas wanaojitanabaisha kulinda masilahi ya Palestina katika Ukanda wa Gaza walikubaliana kusitisha mapigano ili kuruhusu mazungumzo na huduma za kibinadamu kuwafikia wananchi wa Gaza.

Hata hivyo, pande mbili hizo zilifufua mapigano, huku kila mmoja ukiutaja mwingine kukiuka makubaliano. Israel ilitajwa kutokuondosha wanajeshi wake Gaza kama ilivyotakiwa katika makubaliano hayo.

Tangu hapo, Israel imeripotiwa kuua Wapalestina zaidi ya 1,200, pia ikijiongezea maeneo ya kutawala katika Ukanda wa Gaza.

Aidha, Wapalestina zaidi ya milioni mbili hawana makazi au wanaishi kwenye kambi za wakimbizi, ambako hali ni mbaya kutokana na mrundikano unaosababisha magonjwa.

Hivyo, kwa wakazi wa Gaza walio wengi, si Israel wala Hamas inayopaswa kuaminika kwa asilimia 100 kwani pande zote mbili hazioneshi utayari wa kurejesha amani katika eneo hilo.

Hilo lilithibitishwa na kauli aliyowahi kuitoa Waziri Mkuu wa Israel, Banjemin Netanyahu, aliposema: “Israel haitoondoa wanajeshi wake (Gaza). Tunataka kuiteka moja kwa moja.”

Pia, inaelezwa kuwa si raia wote wa Palestina wanaiamini na kuiunga mkono Hamas, lakini hawapingani nayo kwa kuwa inapigana na Israel, ambao ni maadui wao wakubwa.

Iko hivyo pia kwa Israel, ambako si raia wote wanavutiwa na kinachofanywa na Serikali yao katika Ukanda wa Gaza, lakini wanatamani kuona wakiwatawala Wapalestina na nchi zote zinazoongozwa kwa misingi ya Dini ya Uislam.

Related articles

Recent articles