28 C
New York

Urusi v Ukraine: Mawaziri, wakuu wa majeshi viti havikaliki

Published:

KYIV, Ukraine

HIVI karibuni, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, alimfuta kazi Mkuu wa Majeshi, jenerali Oleksandr Syrskii, siku chache baada ya ‘kumtumbua’ Waziri wa Ulinzi, Mykhailo Fedorov.

Syrskii (60), akipachikwa jina la ‘Shujaa wa Ukraine’ kwa namna alivyokabiliana vizuri na Urusi tangu vita kati ya mataifa hayo vilipoanza Februari, 2022.

Ndiye aliyesimamia operesheni ya kurejesha kwenye udhibiti miji mikubwa miwili, Kupiansk na Izyum, iliyokuwa imetekwa na Urusi.

Kwa sasa, nafasi yake ya Mkuu wa Majeshi imechukuliwa na jenerali Mykhailo Drapatyi.

Kwa upande mwingine, miaka minne ya vita dhidi ya Urusi imeshuhudia Ukraine ikifanya mabadiliko kadhaa kwenye nafasi ya Mkuu wa Majeshi na ile ya Waziri wa Ulinzi.

Septemba, 2023, Rais Zelenskyy alimuondosha Waziri wa Ulinzi, Oleksii Reznikov, kutokana na skendo za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Februari, 2024, Rais Zelenskyy ‘alimtumbua’ Mkuu wa Majeshi, Valerii Zaluzhnyi, na nafasi yake kuchukuliwa na Syrskii.

Kwa upande wake, Urusi nayo nayo imefanya mabadiliko kadhaa, yakiwamo ya Agosti, 2022, ambapo aliyekuwa kiongozi wa operesheni ya Bahari Nyeusi, Igor Osipov, alifutwa kazi.

Julai, 2023, Meja Jenerali Ivan Popov, ambaye alikuwa akisimamia operesheni za Kusini mwa Ukraine, naye alipoteza kibarua, akikosolewa kwa mbinu zake za vita, pia kutowapa muda wa kupumzika wanajeshi wake.

Agosti, 2023, Serikali ya Rais Vladimir Putin ilitangaza kumfuta kazi aliyekuwa kiongozi wa jeshi la anga, Sergey Surovikin.

Related articles

Recent articles