Na mwandishi wetu, Gazetini
BILIONEA Elon Musk, ambaye ndiye mmiliki wa X [zamani Twitter], ndiye mtu mwenye wafuasi wengi zaidi katika mtandao huo wa kijamii. Wafuasi [followers] milioni 242.
Musk aliununua mtandao huo mwaka 2022 kwa Dola bilioni 44, wakati huo ukiitwa Twitter na Obama akiwa ndiye mtu mwenye wafuasi wengi. Tajiri huyo alibadili jina na kuuita ‘X’ mwaka 2023.
Kwa idadi hiyo ya wafuasi milioni 242, Musk amewazidi Barack Obama na Cristiano Ronaldo, ambao wanashika nafasi ya pili na ya tatu kwa idadi kubwa ya ‘followes’ kwenye mtandao huo.
Obama anayeshika nafasi ya pili, ana wafuasi milioni 119, akifuatiwa na Ronaldo [milioni 114], Donald Trump [milioni 112], na mwanasia wa India, Narendra Modi [milioni 107].
Katika nafasi ya sita ni wanamuziki Rihanna [milioni 99], Justin Bieber [milioni 92], Katy Perry [milioni 90], Taylor Swift [milioni 84], Lady Gaga [milioni 75], na staa wa kriketi nchini India, Virat Kohli [milioni 73].
Wengine ni mtangazaji wa vipindi vya runinga, Kim Kardashian [milioni 71], mwanasoka Neymar [milioni 66], mfanyabiashara Bill Gates [milioni 65], na mwanamuziki Selena Gomez [milioni 63].


