Na mwandishi wetu, Gazetini
UGIRIKI na Japan ndizo nchi zinazotajwa kuwa na kipimo kigumu zaidi kwa dereva kukabidhiwa leseni na kuingia barabarani.
Kwa Ugiriki, dereva anayehitaji leseni ya udereva atafanya mtihani wenye maswali 30 ndani ya dakika 35 tu. Katika mtihani huo, atahesabika amefaulu endapo atapata maswali 29. Akose moja tu!
Mtihani huo utahusisha maswali yanayohusu uelewa wa dereva juu ya alama za barabarani, usahihi wa njia, udhibiti wa mwendo, usalama wa chombo [gari], na sheria zingine za barabarani.
Ni kutokana na ilivyo ngumu kupata leseni, Ugiriki ilikuwa na vifo 6.1 tu vya ajali za barabarani kwa kila watu 100,000, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023.
Kwamba Ugiriki ndiyo nchi pekee ya Umoja wa Ulaya [EU] iliyokuwa na vifo vichache vitokanavyo na ajali za barabarani.
Kwa upande wa Japan, ili kupata leseni ya Daraja B, dereva atalazimika kupata asilimia 95 katika mtihani wake. Mtihani huo huwa na maswali ya nadharia na vitendo.
Nchi zingine zenye viwango vya juu vya ufaulu wa mitihani ya kupata leseni za udereva ni Vietnam [91%], New Zealand [91%], Australia [91%], Hispania [90%], na Italia [90%].
Bila kusahau, kuna Ukraine [90%], Iceland [90%], Luxembourg [90%], Kuwait [90%], Qatar [90%], Singapore [90%], Latvia [90%], na Ureno [90%].


