28 C
New York

Urusi inasiaidia Iran kuitandika Marekani?

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

HIVI karibuni, Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Marco Rubio, alikuwa Manila, Ufilipino, ambako alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

Moja ya ajenda katika mazungumzo yao ikawa ni vita inayoendelea kati ya Urusi na majirani zao wa Ulaya Mashariki, Ukraine.

Hata hivyo, Rubio na Lavrov walikutana wakati huu zikiwepo taarifa zinazodai kuwa Urusi imejitosa kimyakimya kuisadia Iran katika vita vyake dhidi ya Marekani.

Kwamba Urusi inasiaidia Iran kutekeleza mashambulizi dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani zilizoko katika nchi za Mashariki ya Kati.

Iran ilianza kushambulia kambi za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) zilizoko Oman, Qatar na nchi zingine jirani tangu vita vilipoanza Februari 28, 2026.

Machi 3, 2026, kambi ya Marekani iliyoko mjini Riyadh, Saudi Arabia, ilishambuliwa na ndege zisizo na rubani za Iran.

Siku tatu baadaye, ndipo kituo cha televisheni cha CNN kilipoibua madai kuwa Urusi imekuwa ikiisaidia Iran kuratibu mashambulizi hayo.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, chombo kingine cha habari cha Reuters kiliripoti kuwa Marekani imeanza uchunguzi juu ya uwezekano wa Urusi kuhusika katika mashambulizi ya Iran.

Mchambuzi wa siasa, Nicole Grajewski, ambaye pia ni mhadhiri wa moja ya vyuo vikuu jijini Paris, anaamini Urusi imetia mkono katika vita hivyo.

“Dhana hiyo inatokana na ukweli kwamba mashambulizi ya sasa ya Iran ni ya kisasa zaidi kuliko wakati ule vita vinaanza,” amesema.

“Iran haina idadi kubwa ya setilaiti za kivita kama ilivyo Urusi. Inaonekana imeanza imeingia makubaliano ya kusaidiana na Urusi.”

Lakini, hoja yake hiyo inapingwa na baadhi ya wachambuzi wanaoamini Israel iko mbali katika teknolojia ya silaha za kivita, hivyo haiitegemei Urusi kuisumbua Marekani.

Aidha, tangu Urusi ilipotengwa na kuwekewa vikwazo na mataifa mengine ya Ulaya, ukaribu wake na mamlaka za Iran umeripotiwa kuongezeka mara dufu.

“Nchi zote mbili zinajichikulia kama wahanga (dhidi ya Magharibi). Ushirikiano wao kijeshi ulianzia pale Urusi ilipoivamia Ukraine na sasa umeongezeka zaidi,” amesisitiza Grajewski.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, baada ya kuivamia Ukraine, Urusi ilipokea msaada wa idadi kubwa ya silaha za kivita kutoka Iran. Moja ya hizo ni ndege zisizo na rubani aina ya Shahed.

Mwaka 2025, pande mbili hizo zilisaini mkataba wa kushirikiana kimkakati, hasa katika maeneo nyeti ya ulinzi na usalama.

Hata hivyo, mara zote Urusi imekanusha kujihusisha na vita vya Marekani na Iran, ikidai kuwa mkataba wake na Taifa hilo la Kiarabu hauhisishi kushirikiana kijeshi.

Wakati huo huo, wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaiona Urusi ikinufaika na mgogoro unaoendelea kati ya Marekani Iran.

Mosi, ni kwa sababu dunia inajikita huko Mashariki ya Kati na kusahau uonevu inaoendelea nao dhidi ya majirani zao, Ukraine.

Pili, Urusi inaamini kuwa vita dhidi ya Iran vinaifanya Marekani iendelee kupoteza nguvu ya kiuchumi na hata ushawishi wake katika siasa za ulimwengu.

Related articles

Recent articles