26.5 C
New York

Trump kuibiwa kura: Madai yake yana ukweli kiasi gani?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KATIKA hotuba yake ya Julai 17, 2026, Rais Donald Trump aliishutumu China kwa kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwaka 2020.

Trump anaamini China ilichezea mfumo wa upigaji kura, hivyo kusababisha abwagwe na Joe Biden katika kinyang’anyiro cha urais.

Hata hivyo, madai yake hayo yanapishana na ripoti za mamlaka ya ulinzi na usalama zilizowahi kutoa tathimini ya Uchaguzi huo.

UKWELI UKO WAPI?

Katika tathimini yake ya mwaka 2021, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lilieleza kuwa China haikufanikiwa kuingilia Uchaguzi wa mwaka 2020.

Tathimini hiyo iliyoongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, John Ratcliffe, ilieleza kuwa ni mwaka 2008, ndipo China ilijaribu kukusanya taarifa za wapiga kura, maoni yao na yale ya vyama vya siasa.

Lakini, kwa mujibu wa CIA, taarifa hizo haziwezi kuathiri matokeo, bali hutumika kutoa picha ya mgombea au chama kinachokubalika zaidi kuelekea Uchaguzi.

Ni kama zilivyofanya Urusi na Brazil zilizotaka Rais Trump ashinde, au Cuba na Venezuela zilizoendesha kampeni za chini chini (siyo kuiba kura) zikitamani Biden aingie madarakani.

KAWAIDA YAKE, UPINZANI WAMVAA

Kama itakumbukwa, Rais Trump aliwahi pia kuushutumu utawala wa Rais Nicolas Maduro nchini Venezuela akisema ‘ulichezea’ Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo baadaye yalikanushwa na ripoti ya CIA.

CIA ilikiri kuwa Maduro na watu wake walichezea mifumo ya upigaji kura lakini kwa lengo la kuibia wapinzani wake wa ndani na si Uchaguzi wa Marekani.

Sasa, kuhusu hili la China, si tu CIA, bali hata Chama cha upinzani cha Democrat nacho hakioni ukweli wa madai hayo ya Rais Trump.

Seneta wa Democrat, Mark Warner, alitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) kumshambulia kiongozi huyo, akiandika:

“Shutuma za Trump dhidi ya China ni upuuzi mtupu. Ukweli ni kwamba vyombo vyetu vya usalama vilishakubaliana kwamba China haikubadili hata kura moja katika Uchaguzi wa mwaka 2020.”

Kwa mtazamo wa Seneta Warner, Rais Trump anajaribu kuyumbisha ukweli kwamba Chama chake cha Republican kinakabiliwa na anguko kubwa katika Uchaguzi ujao wa Novemba, 2026.

CHINA YAMJIBU

Baada ya hotuba ya Rais Trump, Msemaji wa Ubalozi wa China nchini Marekani, Liu Chang, alikanusha madai hayo akisema:

“China kwa muda mrefu imekuwa ikiheshimu misingi yake ya kutokuingilia masuala ya ndani ya nchi zingine. Uchaguzi wa Marekani ni suala la ndani la Marekani.

“Matokeo yake yanapaswa kutokana na kura za Wamarekani. China haijawahi na haitowahi kuingilia Uchaguzi wa rais wa Marekani.”

Related articles

Recent articles