14.3 C
New York

Liverpool yamvalia njuga beki Uholanzi

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KLABU ya Liverpool haijaacha kumfuatilia beki wa kulia anayefanya vizuri Ligi Kuu ya Uholanzi akiwa na kikosi cha Feyenoord, Givairo Read.

Hata hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 ameripotiwa pia kuingia kwenye rada za klabu Arsenal na Manchester City.

Givairo amekuwa moto wa kuotea mbali tangu msimu huu uanze, ambapo ametoa asisti tano katioka mechi saba tu za Ligi Kuu [Eredivisie].

Mlinzi huyo alikaribia kutua England wakati wa usajili wa kiangazi. Klabu za Nottingham Forest na Everton zilijaribu kuinasa saini yake.

Kwa upande wake, Liverpool wanahitaji beki wa kulia kutokana na kushuka na kupanda kwa kiwango cha Jeremie Frimpong.

Ni kutokana na kiwango chake hicho, kocha wa Liverpool, Andoni Iraola, amekuwa akimtumia Ronald Araujo kucheza eneo hilo.

Related articles

Recent articles