14.3 C
New York

Atletico yamjia juu Mourinho

Published:

MADRID, Hispania

KLABU ya Atletico Madrid imemjibu kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, baada ya Mreno huyo kuwatupia lawama waamuzi wa mchezo wao uliopita.

Baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1 katika mechi hiyo ya La Liga, Mourinho alielekeza lawama zote kwa mwamuzi, akisema wapinzani wao hao walipaswa kulimwa kadi nyekundu.

Ikumbukwe, tayari Dean Huijsen wa Madrid alishatolewa kwa kadi nyekundu mwanzoni kabisa mwa mchezo baada ya rafu yake kwa Giuliano Simeone wa Atletico,

Sasa, kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter], Atletico wameandika: “Acha kuwashushia heshima waamuzi.”

Mourinho alivurugwa kwa kuwa hicho kilikuwa ni kipigo cha pili kwa timu yake msimu huu baada ya kufungwa bao 1-0 na Real Betis mwanzoni mwa Septemba, 2026.

Related articles

Recent articles