LONDON, Uingereza
KLABU ya Tottenham imeanza harakati za kuinasa saini ya mshambuliaji wa kati asiye na klabu kwa sasa, Mauro Icardi, kwa mujibu wa mtandao wa Football Insider.
Kwa upande mwingine, Icardi mwenye umri wa miaka 33 anawindwa pia na wakongwe wa Ligi Kuu ya Italia [Serie A, Lazio.
Tottenham watapaswa kusubiri hadi Januari, 2026, ili kuweza kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 33.
Kocha wa Tottenha, Roberto De Zerbi, anahitaji mshambuliaji mpya baada ya timu yake kufunga mabao mawili tu katika mechi tano za msimu huu wa Ligi Kuu ya England.
Icardi hana timu kwa sasa baada ya kuachana na Galatasaray aliyoachana nayo baada ya kuitumikia kwa miaka minne.


