14.3 C
New York

Iran yapewa onyo kali

Published:

NEW YORK, Marekani

UMOJA wa nchi tajiri saba duniani [G7] unaozihusisha Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani, umeitaka Iran kuacha mara moja kusapoti kundi la kigaidi la Houthis la nchini Yemen.

Onyo hilo limekuja kupitia taarifa ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje wa G7 wakilaani mashambulizi makali yanayotokelezwa na wapiganaji wa Houthi huko Saudi Arabia.

Wakati huo huo, maelfu ya raia wa Yemen wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya Houthis kuteka maeneo mengi ya Taifa hilo.

Katika taarifa yao ya pamoja, G7 wameeleza: “Tunaitaka Houthis kuacha mara moja mashambulizi na vitisho dhidi ya meli za raia na kurejea kwenye michakato ya kisiasa.”

Kwa upande mwingine, Umoja huo umesisitiza kuwa bado utaendelea kuiunga mkono Serikali ya Yemen katika mapambano yake dhidi ya Houthi.

Related articles

Recent articles