LONDON, Uingereza
MPACHIKAJI mabao wa zamani wa Watford, Troy Deeney, amemtupia lawama kocha wa Manchester United, Michael Carrick, akisema ndiye chanzo cha mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi msimu huu.
Man United inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa imeshinda mechi moja na kufungwa mbili katika tano walizocheza msimu huu.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha talkSPORT, Deeney anaamini Carrick anang’ang’ania kumtumia Marcus Rashford katika kikosi cha kwanza na hilo ndilo tatizo.
“[Benjamin] Sesko anakosekana, halafu unajaribu kulazimisha Marcus Rashford, ambaye hata hivyo anaonekana ni wa kawaida,” amesema Deeney.
Rashford hajafunga bao wala kutoa ‘asisti’ tangu aliporejea Man United akitokea Barcelona alikokuwa akicheza kwa mkopo.


