14.3 C
New York

Lineker: Tatizo la Chelsea ni mabeki

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Barcelona, Gary Lineker, ameitazama Chelsea na kugundua kuwa shida yao kubwa msimu huu ni safu ya ulinzi.

Chelsea iko chini ya kocha mpya raia wa Hispania, Xabi Alonso, ambaye alikabidhiwa benchi la ufundi mwishoni mwa msimu uliopita [2025-26].

Chini yake, Blues wamecheza mechi saba za mashindano mbalimbali, ambapo ameshinda nne, sare moja na kufungwa mbili.

Kwa upande wake, Lineker raia wa England amesema: “Msingi wa timu kuwa na mafanikio ni safu ya ulinzi iliyo bora.”

Wakati huo huo, Lineker ameipongeza safu ya ushambuliaji ya Blues lakini amesema ni ngumu timu hiyo kupata mafanikio endapo itaendelea kuruhusu mabao.

Related articles

Recent articles