25.3 C
New York

Mabao ya nje ya boksi yaweka rekodi

Published:

MIAMI, Marekani

HATA kabla ya fainali kuchezwa, tayari idadi ya mabao yaliyofungwa kwa mashuti ya nje ya boksi ilishavunja rekodi ya fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2022.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), asilimia 16 ya mabao yaliyofungwa msimu huu yalifungwa kwa mashuti ya nje ya 18.

Ni tofauti na msimu uliopita wa mashindano nchini Qatar, ambapo ni asilimia nane tu ya mashuti ya nje ya boksi yaliyozaa mabao.

Kwa mujibu wa wachambuzi, ongezeko la hilo linaweza kuwa limetokana na timu nyingi ‘kupaki basi’, hivyo wapinzani kujaribu mashuti wakiwa nje ya eneo la penalti.

Mkongwe wa soka la Ujerumani, Jurgen Klinsmann, amesema fainali za mwaka huu zimeshuhudia timu nyingi zikiwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye eneo la ulinzi.

Kwa mujibu wa Klinsmann, wingi huo wa wachezaji kwenye boksi umekuwa ukiathiri uwezo wa makipa kuona mpira, hivyo kujikuta wakiruhusu mabao ya mashuti ya nje ya boksi.

“… Wachezaji nane hadi tisa wanakuwa ndani ya boksi, hivyo ni rahisi kwa wapinzani kupiga wakiwa nje kutokana na ugumu wa kuingia,” amesema.

Kabla ya fainali yao dhidi ya Hispania, Argentina ilikuwa ndiyo timu yenye mabao mengi ya nje ya boksi (5), likiwamo la dakika ya 85 alilofunga Enzo Fernandez katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya England.

Related articles

Recent articles