LONDON, Uingereza
KOCHA wa zamani wa Manchester City, Pep Guardiola, amemtaja Neymar kuwa ndiye mchezaji aliyetamani zaidi kufanya naye kazi.
Wawili hao walipishana Barcelona kwani wakati Guardiola anatua mwaka 2013, tayari Neymar alishaondoka mwaka mmoja kabla.
“Kama kocha, mara zote ningependa kufanya kazi na Neymar,” amesema Guardiola.
Kwa upande mwingine, uwezekano wa Guardiola na Neymar kufanya kazi pamoja kwa sasa ni mdogo.
Neymar ambaye ameshastaafu soka la Kimataifa, bado ni mchezaji wa Santos inayoshiriki Ligi Kuu nchini Brazil.
Guardiola, kwa upande wake, kwa sasa hana timu tangu alipoondoka Manchester City mwishoni mwa msimu uliopita (2025-26).


