LOS ANGELES, Marekani
SUPASTAA wa muziki raia wa Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon, amefichua sababu ya kuachana na Drake na kumsaini Wizkid kwenye lebo yake mwaka 2008.
Kwa mujibu wa Akon, wakati huo Drake hakuwa staa mkubwa lakini alitaka fedha nyingi, yaani Dola milioni moja.
Akon ameeleza kuwa alikutana na Wizkid alipofika Nigeria kukutana na staa mwingine wa Afrobeats, Banky W.
“Banky W ndiye aliyeibua kipaji cha Wizkid. Nilifika Nigeria na yeye ndiye aliyeniletea Wizkid,” amesema Akon.
Akifunguka zaidi, Akon amesema wakati huo Bank W hakuwa na pesa nyingi, hivyo akaamua kuwekeza na huo ukawa mwanzo wa Wizkid kufahamika na kuwika Marekani.


