HARARE, Zimbabwe
RAIS wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameendelea kutetea hatua ya Bunge kubadilisha Katiba na kumpa nyongeza ya kubaki madarakani hadi mwaka 2030.
Wakati huo huo, wanaharakati, demokrasia na wanasiasa wa upinzani na hata baadhi ya wananchi hawajaacha mabadiliko.
Rais Mnangagwa alipaswa kuondoka Ikuku mwaka 2028 lakini mabadiliko yaliyofanyika yatachelewesha Uchaguzi Mkuu, hivyo kiongozi huyo kubaki madarakani kwa miaka miwili zaidi.
Mbali na muhula mmoja wa Rais kuwa miaka saba badala ya mitano, mabadiliko mengine ni pamoja na idadi ya wabunge kuongezeka kutoka 80 hadi 90, pia kiongozi wa nchi kuongezewa nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa.
Kwa upande wake, Rais huyo ameyaita mabadiliko hayo kuwa ni uamuzi wa pamoja wa kisiasa na si matakwa binafsi.
“Haukuwa uamuzi binafsi … Siamini katika ushawishi au mfumo wa mtu mmoja, ambapo matakwa ya mtu yanaamua. Naongoza Baraza la Mawaziri na nchi kwa mujibu wa maamuzi ya pamoja,” amesema.
Hata hivyo, kauli yake hiyo inapingana na ile aliyoitoa Septemba, 2024, wakati wa ziara yake nchini China, ambapo aliahidi hadharani kuwa angeachia madarada baada ya muhula wake wa pili kuisha mwaka 2028.
Lakini, wakosoaji wake wanasema mchakato wa mabadiliko ya Katiba, hasa kipengele cha Rais kuongezewa muda, ulipaswa kuhusisha ukusanyasaji wa maoni ya wananchi.
Pia, wanaonya kuwa mabadiliko hayo yanaweza kuingiza nchi kwenye hali mbaya ya kiusalama, hivyo kurudisha nyuma jitihada za kushawishi wawekezaji wa nje.


