33.7 C
New York

Andrey Santos; Jembe jipya ndani ya Old Trafford

Published:

MANCHESTER, Uingereza

USAJILI wake umekamilika baada ya Manchester United kuipa Chelsea kitita cha Pauni milioni 48. Ni kiungo wa Kibrazil, Andrey Santos.

Man United imeachana na usajili wa Pauni milioni 35 wa ‘mido’ wa Atalanta ya Serie A baada ya vipimo kuonesha ana changamoto ya majeraha.

Santos (23), ametua Old Trafford na kusaini mkataba utakaokwisha Juni, 2031, pia ukiwa na kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja endapo ataonesha kiwango kizuri.

Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Blues kilichotwaa taji la fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu mwaka 2025 na alicheza mechi 43 msimu uliomalizika (2025-26).

AMTAJA CARRICK

Santos hakwenda Kombe la Dunia mwaka huu, hivyo ameshaanza mazoezi na Man United, akisubiri safari ya ‘pre-season’ itakayoanza Julai 18, 2026.

Amemtaja kocha wa Man United, Michael Carrick, akisema anaamini atajifunza mengi kutoka kwa kiungo huyo wa zamani.

“Kama mchezaji wa eneo la kiungo, nimefurahi kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa Michael Carrick. Ni kocha sahihi wa kunisadia kupiga hatua zaidi katika maisha ya soka na kutimiza ndoto zangu,” amesema Santos.

ALIANZIA HUKU

Safari ya maisha yake ya soka ilianzia katika klabu ya Vasco da Gama ya Brazil aliyojiunga na academy akiwa na umri wa miaka minne.

Mwaka 2016, akiwa na umri wa miaka 16, Santos alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya wakubwa.

Chelsea iliinasa saini yake Januari 6, 2023, lakini alirejea kwa mkopo Vasco, kisha kupelekwa Nottingham Forest na Strasbourg ya Ufaransa.

Alirudi Stamford Bridge mwaka 2025 na kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Chelsea katika ushindi wa 3-0 dhidi ya ES Tunis kwenye Kombe la Dunia ngazi ya Klabu.

Santos alifunga bao la kwanza akiwa Chelsea katika mchezo walioshinda mabao 4-3 dhidi ya Wolves.

NAHODHA WA BRAZIL, AKATWA KOMBE LA DUNIA

Santos alikuwa nahodha wa U-20 ya Brazil wakati timu hiyo inatwaa ubingwa wa michuano ya Amerika ya Kusini mwaka 2023. Alifunga mabao sita kwenye mashindano hayo.

Pia, akawa nahodha wa kikosi hicho kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia la U-20 na U-23 iliyocheza michuano ya kujiandaa na Olimpiki.

Mwaka huo huo, akaitwa kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa, wakati huo Ramon Menezes akiwa kocha wa muda baada ya Dunga kuachia ngazi.

Kuelekea fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026), kocha Carlo Ancelotti alimjumuhisha katika kikosi cha awali cha wachezaji 55 lakini alimkata wakati wa kuchagua nyota 26 wa kwenda nao kwenye michuano hiyo.

Related articles

Recent articles