27.4 C
New York

Samatta na viatu vyake, Mwakinyo na glovu zake

Published:

Samatta na viatu vyake, Mwakinyo na glovu zake

Na Hassan Mwasha, Gazetini

SAFARI ya Mbwana Samatta na timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefikia tamati. Alitangaza kustaafu siku chache zilizopita.

Hakuna aliyeshutushwa na wala sijabahatika kukutana na komenti za mashabiki walioumizwa na uamuzi huo wa Samatta.

Kana kwamba walitarajia au wameona amechelewa kuchukua uamuzi huo. Hawaoneshi kuwa alikuwa na nafasi yake muhimu kikosini.

Hata kama si kikosini, basi hawaoni kama Samatta alikuwa na maana yoyote kwenye soka la nchi hii. Inasikitisha.

Hata hivyo, kama ambavyo hawakushitushwa, binafsi pia sikuwashangaa. Na badala yake, niliona Samatta amechelewa mno kujiweka kando na kuendelea na maisha yake.

Iko hivi; kwa makusudi, mashabiki wa soka hapa nchini waliamua kumuweka Samatta katika daraja la wachezaji wa kawaida tulionao kwenye Ligi yetu.

Wakati mwingine, hata kulidikiri kujisahau na kumuona hafiki levo za baadhi ya wachezaji wa ndani waliochagua kuwapenda. Inashitua.

Samatta ambaye ndiye Mtanzania pekee kuwahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (akiwa TP Mazembe mwaka 2015) lakini kwa mashabiki wa Bongo, akaonekana wa kawaida tu.

Mchezaji ambaye ndiye Mtanzania pekee katika historia ya soka la nchi hii kubeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Ndani wa CAF (2015) lakini akakosa heshima yake kwa mashabiki wa nyumbani.

Akaonekana wa kawaida licha ya kuwa mchezaji pekee kutoka Bongo kukipiga Ligi Kuu ya England (EPL). Huyo ndiye Samatta na hao ndiyo mashabiki wa soka la Bongo.

Unazungumzia mchezaji anayetokea katika nchi isiyo na miradi bora ya kuibua na kuendeleza vipaji.

Nchi ambayo klabu zake kubwa, Simba na Yanga, zimeishia kuwa wasindikizaji kwenye michuano yote ya ndani ya Afrika, kama ilivyo kwa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Katika mazingira hayo, Samatta ameweza kuibuka shujaa na kuipeleka Tanzania kimataifa, akianzia DRC, kisha Ligi Kuu za Ublegiji, Uingereza, Uturuki na Ufaransa.

Unamchukuliaje poa mchezaji wa aina hiyo? Unamfananisha na nani kati ya waliopo sasa kwenye soka la nchi hii?

Samatta anaweza akawa hakufikia matarajio waliyokuwa nayo mashabiki wa Stars lakini je, walitarajia kuona mchezaji anayetoka nchi hii ya viwango vya chini vya ubora wa soka akicheza Aston Villa? Mbali ya mengine, walipaswa kuheshimu hilo pia.

Kwa upande mwingine, kuna mstari mwembamba mno unaotofautisha maisha ya Samatta na anayoishi bondia Hassan Mwakinyo.

Mwakinyo anaweza kuwa na changamoto zake lakini haiondoshi ukweli kwamba ni mmoja kati ya mabondia bora na wenye mafanikio makubwa ndani ya nchi hii.

Licha ya Tanzania kutokuwa na uwekezaji wa maana kwenye ngumi, hali ambayo pia pia kwa upande wa soka, bado Mwakinyo amepenya na kujenga heshima yake na ya nchi kwenye medani ya kimataifa.

Katika mazingira ambayo ungedhani angepata uungwaji mkono mkubwa, Mwakinyo amekuwa ‘adui wa wengi’ ndani ya tasnia. Hii inashangaza.

Vipi Mwakinyo na Samatta wangekuwa raia wa kigeni? Ni wazi wangepata heshima kubwa hapa nchini, kama ilivyo kawaida ya Watanzania kumezwa na ulimbukeni.

Mwakinyo na Samatta ni mfano mdogo tu. Tatizo hili la kutukuza wageni limekuwa shimo linalofukia vipaji vingi vya makocha wazawa kwenye soka la nchi hii.Na Hassan Mwasha

Mwakinyo na Samatta ni mfano mdogo tu. Tatizo hili la kutukuza wageni limekuwa shimo linalofukia vipaji vingi vya makocha wazawa kwenye soka la nchi hii.

Related articles

Recent articles