37.6 C
New York

Mwili wa Khamenei wazua gumzo

Published:

TEHRAN, Iran

MAMLAKA za Iran zimetangaza Julai 9, 2026 kuwa ndiyo siku za maziko ya Kiongozi wa zamani wa Taifa hilo, Ali Khamenei, huku ukiibuka mjadala mzito nchini humo.

Ni miezi minne imepita tangu Khamenei aliouawa katika shambulizi la pamoja la Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Sasa, baadhi ya viongozi wa Dini ya Uislam nchini Iran wamekwazika na kitendo cha kiongozi huyo kuchelewa kuzikwa.

Katika hoja yao ya msingi, mwili wa alitefariki upaswa kuzikwa haraka baada ya kifo, hivyo kuchelewa kwa Khamenei ni kinyume cha mafundisho ya Dini yao.

Pia, wanahoji namna mwili wa Khamenei ulivyohifadhiwa tangu Februari 28, 2026, wakitilia shaka utumizi wa kemikali ili usiharibike.

Related articles

Recent articles