37.6 C
New York

‘Ushamba’ huu unaua ‘brand’ anayoipigania Injinia Hersi

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MSIMU wa 2025/26 ulifikia tamati Juni 30, 2026, na habari kubwa ni Yanga kutwaa taji kwa mara ya tano mfululizo.

Kwa ufupi, Yanga imekuwa bingwa wa michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu tangu msimu wa 2021-22.

Nini siri ya Yanga? Ukiniuliza, nitakwambia hivi; siri ya Yanga kwa misimu yote mitano ya hivi karibuni ni nguvu kubwa ambayo viongozi wamekuwa wakiiweka.

Achana na usajili wa wachezaji sahihi. Achana na malipo mazuri ya mishahara na posho. Achana pia na kambi nzuri.

Kumuona Rais wake, Injinia Hersi Said, akiwa jukwaani katika kila mechi, zikiwamo zilizoonekana za kawaida, ni kielelezo kikubwa cha ‘usiriazi’ wa uongozi wa Yanga katika kile inachopigania.

Uwepo wake jukwaani ulituma ujumbe kwenye vichwa vya wachezaji, kwamba uongozi wa Yanga unaupa kipaumbele kila mchezo, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanavuja jasho jingi na kushinda.

Matokeo yake, Yanga imekuwa timu pekee ndani ya misimu mitano mfululizo kuwa washindi wa mbio za ubingwa wa Ligi na safari hii taji limekuja ikiwa imefungwa mechi moja tu.

Tutoke huko. Eneo jingine ambalo Yanga imefanya vizuri ni katika ‘branding’. Weledi wa viongozi wa sasa umeiongezea thamani kubwa nembo ya klabu.

Kuthibitisha hilo, unaweza kuona idadi kubwa ya wadhamini iliovuna ndani ya kipindi hiki cha uongozi wa Injinia Hersi.

Kwa uzoefu wa kibiashara, hutegemei kuona wadhamini wakipishana mlangoni kuingia katika chapa isiyoshawishi.

Hivyo, kuona Yanga ikiwa na wadhamini wengi ni matokeo ya kazi kubwa ya kuing’arisha nembo ya Yanga na kuifanya iwe na mvuto kwa kampuni zilizolipa fedha nyingi ili kuitumia kujitangaza.

Hata hivyo, lipo tukio moja lililojirudia mara mbili msimu huu, likibeba picha ya aibu, pamoja na kuitia doa nembo ya Yanga.

Katika mchezo wa mwisho wa msimu huu dhidi ya JKT Tanzania, Yanga walirudia kitendo cha kutokutumia vyumba vya kubadilishia nguo vya Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo.

Na badala yake, ‘Wananchi’ walichagua kuingia na kufanya maandalizi yao kwenye nyumba iliyopo jirani na Uwanja huo. Ilishangaza!

Mosi, ni kwa sababu tukio hilo limejirudia baada ya awali kujitokeza katika Uwanja huo huo, mechi yao ya ‘Kariakoo Derby’ dhidi ya Simba.

Pili, kwa klabu ya hadhi kubwa kama Yanga, ungetarajia kuona ikiwa mfano wa kuigwa katika kuheshimu misingi ya weledi, tofauti na hicho kilichotokea.

Related articles

Recent articles