CARACAS, Venezuela
MTOTO wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu ni miongoni mwa waliookolewa katika operesheni inayoendelea baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba Venezuela.
Taarifa za mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Klieber Moran zimeripotiwa na timu ya uokoaji kutoka Jordan.
Kwa mujibu wa timu hiyo, Moran alikutwa kwenye kifusi katika moja ya majengo kwenye Jimbo la La Guaira.
Katika taarifa yake, Rais wa muda wa Venezuela, Delcy Rodriguez, amesema kupatikana kwa mtoto huyo ni faraja kwa watu wa nchi hiyo.
Wakati huo huo, idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko hilo imefikia watu 1,943, huku zaidi ya 10,000 wakijeruhiwa.
Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa (UN) ulieleza kuwa watu zaidi ya 10,000 wanahitaji msaada kwa sasa.


