MANCHESTER, Uingereza
BABA mzazi wa Erling Haaland, Alfie Haaland, amesema hakuna kocha wa kufikia daraja la Pep Guardiola.
Alfie ametoa kauli hiyo baada ya Man City kumtangaza Enzo Maresca kuwa kocha wake mpya wa msimu ujao (2026-27).
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea anachukua nafasi ya Guardiola aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliomalizika (2025-26).
“Hakuna wa kuziba pengo la Pep Guardiola lakini ni ukurasa mpya wa Man City,” amesema Alfie.
“Inaonekana kama Enzo Maresca atachukua nafasi yake. Ni chaguo zuri, ingawa hakuwa na msimu mzuri (Chelsea) …”


