20.3 C
New York

Matetemeko mawili makubwa yatikisa Venezuela

Published:

CARACAS, Venezuela

MJI mkuu wa Venezuela, Caracas, mapema leo umetikiswa na matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyotokea kwa tofauti ya sekunde chache, hali iliyozua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi na kusababisha hofu ya maafa makubwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS), tetemeko la kwanza lenye ukubwa wa 7.2 lilitokea katika eneo la Montalbán, lililopo magharibi kidogo mwa Caracas.

Sekunde 39 baadaye, tetemeko la pili lenye ukubwa wa 7.5 liliripotiwa kupiga eneo hilo hilo, takribani kilomita 10 kutoka kitovu cha tetemeko la kwanza.

Matetemeko hayo yameelezwa kuwa miongoni mwa matukio makubwa zaidi ya aina hiyo kuwahi kuikumba Venezuela katika kipindi cha karibu karne moja.

Mashuhuda wanasema baadhi ya majengo yaliporomoka huku mamia ya wakazi wakikimbilia barabarani na maeneo ya wazi kutafuta usalama wakati ardhi ilipoanza kutikisika.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodríguez, ametangaza hali ya hatari, wakati juhudi za uokoaji zikiendelea katika maeneo yaliyoathirika.

Hadi sasa, mamlaka hazijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi ya waliopoteza maisha, majeruhi au kiwango halisi cha uharibifu, lakini hofu imeongezeka kuwa watu kadhaa huenda wamekwama chini ya vifusi.

Timu za waokoaji zimeanza operesheni za dharura kutafuta manusura, huku wananchi wakihimizwa kuwa waangalifu kutokana na uwezekano wa mitetemeko mingine kufuatia tukio hilo.

Related articles

Recent articles