20.3 C
New York

Liverpool yamfukuzia beki Korea ya Kusini

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KLABU ya Liverpool imeanza harakati za kumsajili beki wa timu ya Taifa ya Korea ya Kusini, Lee Han-beom, ambaye pia anawindwa na Chelsea.

Nyota huyo wa FC Midtjylland ya Denmark, alikuwa kikosini wakati Korea ya Kusini ilipoanza vizuri msimu huu wa Kombe la Dunia kwa kuifunga Jamhuri ya Czech mabao 2-1.

Lee (23), ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri Ligi Kuu ya Denmark akiwa na FC Midtjylland aliyojiunga nayo mwaka 2023 akitokea FC Seoul ya nchini kwao.

Kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, alifunga bao pekee lililoipa Midtjylland taji la Kombe la Ligi nchini Denmark katika mchezo wa fainali dhidi ya FC Copenhagen.

Amebakiza miezi 12 katika mkataba wake na klabu hiyo na kwa mujibu wa ripoti, Newcastle United na Brighton nazo zinajaribu kuinasa saini yake.

Related articles

Recent articles