BEIJING, China
IKIWA ni miaka miwili imepita tangu alipohukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bosi wake, mwanasheria Xu Yao amenyongwa leo Mei 28, 2026.
Xu alimuua bilionea Lin Qi mwaka 2020 baada ya kumpa vidonge vyenye sumu, ingawa alimdanganya ni vya kinga ya mwili na kurahisisha mmeng’enyo wa chakula.
Inaelezwa kuwa Xu alimpa vidonge hivyo mmiliki huyo wa Kampuni ya Three Body Universe wiki chache tu baada ya dili lao la kufanya kazi na Netflix.
Akiwa kwenye gari lake akirejea nyumbani baada ya kutumia vidonge hivyo, alisijikia vibaya na kwenda hospitali, ambako alifariki siku 10 baadaye akiwa na umri wa miaka 39.
Uchunguzi wa kitaalamu ulibaini kuwa kulikuwa na aina tano za sumu katika mwili wa tajiri huyo.


