Na Editha William Gazetini – KAGERA
MCHEZO wa fainali ya michuano ya soka ya Muhaj Cup 2026 utatanguliwa na bonanza la vijana wa bodaboda kutoka Kata ya Hamgembe iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Ikumbukwe, fainali yenyewe itazikutanisha Mchikichini FC dhidi ya Omukishenye na inatarajiwa kuchezwa wikiendi hii, Novemba 29, 2026.
Mchikichini walitinga fainali baada ya kuifunga Fenicha FC mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa ndani ya dakika 90.
Mchezo huo wa jana Novemba 25, 2026, ulishuhudiwa na Diwani wa Kata ya Hamgembe, Muhaj Kachwamba Abubakari, ambaye amekuwa mdau mkubwa wa mashindano hayo.
Kwa upande wao, Omukishenye walikata tiketi ya fainali walipopata ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Kashabo FC katika nusu fainali ya kwanza.
Hivyo, Fenicha FC na Kashabo zitakwaana katika mchezo wa kusaka mahindi wa tatu utakaochezwa siku hiyo ya fainali.


