CATALUNYA, Hispania
STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, amepata ajali ya gari akiwa njiani kuelekea mazoezini asubuhi ya leo Novemba 26, 2026.
Aubameyang, nyota wa zamani wa Arsenal na Barcelona, kwa sasa anakipiga nchini Hispania akiwa na Deportivo La Coruna.
Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ni gari lake kugogangana na jingine, ingawa hakuumia na baadaye aliweza kujumuhika na wenzake mazoezini.
“Ilitisha kidogo lakini wote ni wazima na hicho ndicho kitu muhimu zaidi,” amesema Aubameyang kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
“Ni kawaida kwenye maisha. Muhimu ni kwamba hakuna aliyeumia. Mambo mazuri huja baada ya nyakati ngumu.”


