15.6 C
New York

Sababu 3 za Chelsea kumtimua Rosenior

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya mfululizo wa matokeo mabaya na kiwango kisichoridhisha cha timu yao, mabosi wa Chelsea walimfuta kazi kocha Liam Rosenior hivi karibuni.

Alifukuzwa baada ya Chelsea kufungwa mabao 3-0 na Brighton, wiki moja tangu uongozi wa klabu hiyo kusema una imani na kocha huyo, licha ya matokeo mabaya.

MAJANGA YA NDANI YA UWANJA

Ni moja ya sababu za kocha huyo kupoteza ajira. Katika mechi 23 alizoinoa Chelsea, ameshinda 11 pekee.

Kichapo kutoka kwa Brighton kilikuwa cha tano mfululizo kwa Blues kwenye Ligi. Ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kukosa ushindi muda mrefu kiasi hicho tangu mwaka 1912.

WACHEZAJI HAWAKUMTAKA

Baadhi ya mastaa wa Chelsea waliripotiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na kocha huyo mwenye umri wa miaka 41.

Enzo Fernandez na Marc Cucurella ni miongoni mwao na mara kadhaa walieleza nia yao ya kuondoka Stamford Bridge.

PRESHA YA KUKOSA LIGI YA MABINGWA

Mabosi wa Chelsea walitangaza hasara ya Pauni milioni 262.4 katika Mwaka wa Fedha uliopita (2024-25).

Moja ya njia za kufidia hasara hiyo ni kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Wakitazama msimamo wa Ligi, wako nje ya ‘Top 5’ kwa tofauti ya pointi saba, jambo lililowaongezea presha na kuamua kumtimua Rosenior.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img