MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Liverpool iko katika hatua nzuri ya kumsainisha mkataba mpya beki wake wa kati raia wa Ufaransa, Ibrahima Konate.
Konate alijiunga na Liverpool mwaka 2021 akitokea RB Leipzig na tangu hapo amekuwa mchezaji tegemeo kikosini.
Akicheza ‘pacha’ na Virgil van Dijk, nyota huyo amecheza mechi 29 za Ligi Kuu ya England msimu huu. Amefunga bao moja.
Wakati huu akielekea ukingoni mwa mkataba wake, Konate amekuwa akihusishwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid.
Hata hivyo, mtandao wa TEAMTalk umeripoti kuwa mlinzi huyo anavutiwa zaidi na mpango wa kubaki Anfield.


