9.5 C
New York

Newcastle kubeba straika Madrid

Published:

MADRID, Hispania

NEWCASTLE United imeingia kwenye harakati za kumsajili straika wa Real Madrid, Gonzalo Garcia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, amecheza mechi 32 za mashindano mbalimbali msimu huu, akifunga mabao sita na kutoa ‘asisti’ mbili.

Garcia alihusishwa na mpango wa kuondoka mwaka jana lakini Madrid waliamua kumpa mkataba mpya utakaokwisha mwaka 2030.

Kwa upande wao, Madrid wako tayari kumwachia kwa mkopo na si kumpiga bei moja kwa moja.

Wakati huo huo, Aston Villa na Besiktas nazo zinatajwa kuitolea macho saini ya nyota huyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img