16.3 C
New York

Mtoto wa Beckham ‘atatoboa’ kimuziki?

Published:

MIAMI, Marekani

ANAITWA Cruz Beckham. Ni mtoto wa mwisho wa kiume wa staa wa soka, David Beckham. Kwake, soka halijawa njia sahihi, na badala yake amechagua kuwa mwanamuziki. Je, ‘ataoboa’?

Cruz (21), ni kiongozi wa bendi yao ya muziki wa Rocky na tayari imeshaanza kufanya shoo nchini Uingereza na barani Ulaya kwa ujumla.

Shoo yao ya wiki hii mjini Birmingham imekuwa gumzo kubwa kutokana na namna ilivyowavuta mashabiki wengi.

Cha kushangaza zaidi, kati ya shoo zake 10 zijazo za Uingereza, nane zimeshafunga hesabu za mauzo ya tiketi.

Tofauti na baba yake aliyejizolea umaarufu mkubwa akiwa mwanasoka aliyecheza Manchester United, Real Madrid na PSG, ‘dogo’ ameamua kufuata nyayo za mama yake, Victoria Beckham ‘Posh’.

Kama itakumbukwa, Posh aliwahi kutamba kwenye soko la muziki duniani akiwa na mmoja ya memba wa Kundi la ‘Spice Girls’.

Hata wakati Cruz na wenzake wanatumbuiza mjini Birmingham, mmoja ya mashabiki alikuwa amevaa ‘t-shirt’ yenye maandishi yanayosomeka ‘POSH’.

Kwa upande wa Posh, ameonesha kuridhishwa na uwezo wa kuimba alionao mwanaye huyo, akimfananisha na staa wa muziki, Justin Timberlake.

Hata hivyo, Cruz kwa upande wake anajiona ni mfano wa supastaa mwingine wa muziki, John Lennon. “Huyo ndiye ninayeiga nyayo zake,” amesema.

Licha ya uchanga wake kwenye gemu, tayari nyota yake imeanza kung’ara, ambapo amesainiwa na lebo ya Republic Records, ambayo inawasimamia mastaa kibao, wakiwamo Taylor Swift na The Weeknd.

Lakini, wakati wengine wakiona umaarufu wa wazazi utambeba, wapo wanaoamini kuwa unaweza kuwa kikwazo kwake kufikia matarajio aliyonao kwenye muziki.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img