9 C
New York

Kocha Harambee Stars ahofia ‘Kundi la Kifo’ AFCON 2027

Published:

NAIROBI, Kenya

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, Benni McCarthy, amesema kupangwa kundi gumu kunaweza kutibua ndoto zao za kufanya vizuri katika fainali zijazo za AFCON 2027.

Droo ya hatua ya makundi haijachezeshwa lakini Kenya ni sehemu ya wenyeji watatu wa michuano hiyo ikishirikiana na majirani zao wa Afrika Mashariki, Tanzania na Uganda.

McCarthy, ambaye ni straika wa zamani wa Bafana Bafana, amefichua kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuvuka hatua ya makundi, ingawa wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi.

“Kenya ni nchi changa, lakini vipaji nilivyoviona hapa ni vikubwa mno. Tunaweza kupiga hatua ambayo Taifa halijawahi kufika,” amesema.

Harambee Stars imeshiriki mara sita fainali za AFCON, ikifanya hivyo mwaka 1972, 1988, 1990, 1992, 2004 na 2019.

Lakini, kwa mara zote hizo, haijawahi kutokea kwa timu hiyo kuvuka makundi na kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img